Category: event
Eneo Lingine Ambalo Tspca Walitembelea Kwaajili Ya Ukaguzi Ni Kampuni Ya Oilcom Ambao Ni Wafugaji Wa ngo’mbe, Farasi, Mbuzi, Kondoo Kwaajili Ya Biashara.
Tumetembelea maeneo ya malisho, majosho, sehemu ya mazalisho, sehemu wanakotunzwa ndama wadogo, sehemu wanakolazwa wanyama wagonjwa, maeneo wanakotunza chakula cha wanyama nk. kifupi shamba linaridhisha isipokuwa yapo maboresho madogo tumewaagiza wafanye kwaajili ya ustawi wa wanyama. ukaguzi utaendelea tena baada ya miezi miwili. Share this…FacebookGoogle+TwitterLinkedin
Tspca Inafanya Ukaguzi Katika Makampuni Yanayofuga Wanyama Kwa Njia Ya Kibiashara.
Dar Es Salaam Zoo. TSPCA imekuta mazingira mazuri, wanyama wanaishi katika mazingira asilia, chakula kipo cha kutosha na maji yapo ya kutosha. TSPCA imewazadia hati maalum ya utunzaji mzuri wa wanyama. ukaguzi huu ni wa kipindi cha miezi sita kwanzia January hadi June 2019. Share this…FacebookGoogle+TwitterLinkedin
Tspca Imefanya Ziara Kwenda Baadhi Ya Mikoa Kukagua Maisha Halisi Ya Mifugo Mbalimbali Na Kuangalia Ni Kwa Kiwango Gani Ukatili Kwa Wanyama Unafanyika.
Ni kijiji kimoja wapo kati ya Dodoma na Babati, tumekuta Ng’ombe wananyweshwa maji katika bwawa chafu sana, TSPCA iliwapa elimu wafugaji kutoendelea kunywesha mifugo katika bwawa hilo. Tspca ilikutana na Punda katika msafara huo wamebebeshwa mizigo bila kuwekewa (Harness) shingoni mwao na wakati huohuo shingo zikiwa zimeshatoka vidonda. Tuliwapa elimu na kuwalazimisha waondoshe hiyo mizigo kwa punda hao haraka sana. Share this…FacebookGoogle+TwitterLinkedin
Kampeni Ya Chanjo Kata Ya Zogohali Ilala.
TSPCA pia inatoa huduma ya kuosha mabanda ya mbwa iwapo tutayakuta ni machafu ambayo ni hatari kwa wanyama kuambukizwa magonjwa. TSPCA inatoa huduma ya kutibu vidonda vya wanyama waliojeruhiwa na watu wasiojulikana na wasiokuwa na huruma. Tspca inatoa pia huduma za kutibu majumbani (mobile clinic) pamoja na kuogesha mbwa. Share this…FacebookGoogle+TwitterLinkedin
- 1
- 2