Tspca Imefanya Ziara Kwenda Baadhi Ya Mikoa Kukagua Maisha Halisi Ya Mifugo Mbalimbali Na Kuangalia Ni Kwa Kiwango Gani Ukatili Kwa Wanyama Unafanyika.

Ni kijiji kimoja wapo kati ya Dodoma na Babati, tumekuta Ng’ombe wananyweshwa maji katika bwawa chafu sana, TSPCA iliwapa elimu wafugaji kutoendelea kunywesha mifugo katika bwawa hilo.

Tspca ilikutana na Punda katika msafara huo wamebebeshwa mizigo bila kuwekewa (Harness) shingoni mwao na wakati huohuo shingo zikiwa zimeshatoka vidonda. Tuliwapa elimu na kuwalazimisha waondoshe hiyo mizigo kwa punda hao haraka sana.